Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya
wametolewa katika michuano hiyo wakati magoli mawili ya Antoine Griezmann
yakiibeba Atletico Madrid na kutinga katika nusu fainali za michuano hiyo.
Barcelona iliwasili katika Jiji la Madrid ikiwa na
ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa awali lakini uzembe wa mabeki wake
ulimfanya Griezmann ambaye alikuwa hana mtu wa kumkaba kupachika bao la kwanza
na kisha baadaye kupachika la pili kwa penati.
Katika mchezo mwingine Bayern Munich ilifanikiwa
kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kupambana na kiume na Benfica
na kutoka sare ya mabao 2-2.
Timu hiyo ya Ureno iliyokuwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi
ya Bayern Munich katika mchezo wa awali, walijipa matumaini baada ya Raul
Jimenez kupachika bao la kwanza katika mchezo wa jana.
Hata hivyo Arturo Vidal na Thomas Muller walifunga
magoli na kuiweka klabu hiyo ya Ujerumani katika nafasi ya kusonga mbele licha
ya Talisca kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 2-2.






0 comments:
Post a Comment