Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ya jijini Dar es
Salaam imemwachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Tanesco William Mhando na wenzake
Sita walioshtakiwa kwa matumizi mabaya kwa kukosa ushahidi.
William Mhando, mke wake Eva Mhando, na wenzao
watatu, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es
Salaam tarehe 27,May 2014, wakikabiliwa na mashitaka sita ikiwemo matumizi
mabaya ya madaraka, kughushi na kujipatia Sh. Milioni 31.7 kwa njia ya
udanganyifu.
Mwendesha Mashitaka wa Taasisi wa Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai kuwa kati ya Aprili Mosi na
Desemba 31, mwaka 2011 katika ofisi za Makao Makuu ya Tanesco jijini Dar es
Salaam, Mhando akiwa mwajiriwa kama Mkurugenzi wa shirika hilo, alitumia vibaya
mdaraka yake.
Alidai kuwa, Mhando alitumia vibaya madaraka yake
kwa kuangalia maslahi yake binafsi baada ya kuipa zabuni ya kusambaza vifaa vya
ofisi kampuni hiyo inayongozwa na mke wake, Eva na watoto wake,vyenye thamani
ya Sh. Milioni 884.5 na kuisababishia kampuni hiyo kupata faida ya Sh. 31,747,000
kinyume cha sheria .
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa kati ya
Januari 6 na Julai 30, mwaka 2011, mahali pasipofahamika, jijini Dar es Salaam,
Eva alighushi taarifa ya ukaguzi wa fedha ya Kampuni ya Santa Clara Ltd,
akionyesha kwamba imekaguliwa na Finx Capital House Desemba mwaka 2010.
Swai alidai katika shitaka la tatu, Agosti 9, mwaka
2011 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Eva alighushi nyaraka za umiliki wa hisa
kutoka Santa Clara Supplies Ltd kwenda Eveta John Shing’oma huku akijua siyo
kweli.
Upande huo wa Jamhuri ulidai katika shitaka la nne,
Agosti 5, mwaka 2011 katika ofisi za Makao Makuu ya Tanesco, jijini, mshtakiwa
Eva aliwasilisha nyaraka za manunuzi za kughushi akionyesha kwamba taarifa hiyo
imeandaliwa na Finx Capital House huku akijua siyo kweli.
Katika shitaka la tano, ilidaiwa kuwa kati ya Aprili
Mosi na Oktoba 31, mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, Eva akiwa kama Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Santa Clara Limited kwa nia ovu, alijipatia faida ya Sh.
Milioni 31.7 kutoka Tanesco baada ya kuwasilisha nyaraka za ukaguzi za
kughushi.
Ilidaiwa katika shitaka la sita, Oktoba 17, mwaka
2011 katika ofisi za Tanesco, mshtakiwa wa tatu hadi wa tano, Mchalange,
Misidai na Kisinga wakiwa watumishi wa shirika hilo, walipokea nyaraka za
kughushi na kusababisha Kampuni ya Santa Clara Supplies Limited kupewa mkataba wa
kusambaza vifaa vya ofisini.
Ilidaiwa kuwa mkataba huo ulisababisha kampuni hiyo
kupata mkataba wa zabuni ya kusambaza vifaa vya Sh. Milioni 884.5 na kupata
faida ya Sh. Milioni 31.5.
Akisoma hukumu hiyo hakimu Hellen Lyimo wa mahakama ya mkazi kisutu amesema kuwa Mahakama haikuwakuta na hatiani washatakiwa hao kwasababu walikuwa hawaingii kwenye vikao vya maamuzi ya zabuni ambayo yalikuwa yanafanywa na bodi ya Tanesco.
0 comments:
Post a Comment