Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa Marekani
(CDC) kimethibitisha kwamba virusi vya Zika husababisha watoto kuzaliwa na vichwa
vidogo na ubongo kudumaa.
Kumekuwa na mjadala mkubwa na suitafahamu kuhusu
uhusiano kati ya virusi hivyo na watoto kuzaliwa na vichwa vidogo tangu
kuongezeka kwa visa vya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Brazil.
Mkurugenzi mkuu wa CDC Tom Frieden amesema hakuna
shaka kwamba virusi vya Zika vinasababisha watoto kuzalwia na vichwa vidogo,
tatizo ambalo kwa Kiingereza hujulikana kama microcephaly.
Maafisa wa CDC wamesema kwamba bado wanawashauri
wanawake wajawazito kutozuru maeneo ya Amerika Kusini na visiwa vya Caribbean,
ambako maambukizi ya virusi hivyo yameripotiwa.
Virusi vya Zika huenezwa sana na mbu ingawa
kumeripotiwa pia visa vya watu kuambukizwa virusi hivyo kupitia kufanya
mapenzi.
Kumeripotiwa visa 346 vya maambukizi ya virusi hivyo
Marekani.
Jumatatu, maafisa nchini humo walionya kwamba
mlipuko wa sasa wa virusi vya Zika huenda ukaathiri sana Marekani na wakaomba
kutolewe ufadhili zaidi.
"Kila kitu tunachofahamu kuhusu virusi hivi
kinaonekana kuwa cha kuogofya zaidi ya tulivyodhania," alisema Dkt Anne
Schuchat kutoka CDC.
Virusi vya Zika viligunduliwa mara ya kwanza mwaka
1947 nchini Uganda, lakini dalili za kuambukizwa virusi hivyo hazijakuwa kali.
Wengi wa wanaoambukizwa walikuwa wakipatwa na homa ambayo si kali sana, mwasho
na maumivu katika maungio.
Mlipuko wa sasa ulianza mwishoni mwa mwaka 2015
nchini Brazil na dalili zake zimekuwa kali.
Watoto karibu 200 wamefariki kutokana na virusi
hivyo.
0 comments:
Post a Comment