Watu wanne wanaarifiwa kufariki dunia kwa kufukiwa na kifusi mara baada ya udongo kuporomoka katika eneo la Ukwamani eneo la Kwandobe Kawe jijini Dar es Salaam Leo.
Watu hao wanaarifiwa kuwa walikuwapo wamelala ndani ya nyumba ndipo wakaporomokewa na udongo ambapo Jeshi la polisi kikosi cha zimamoto na uokoaji pamoja na wananchi wamekuwa na juhudi kubwa za kunasua miili ya waliofukiwa na kifusi cha udongo katika eneo hilo la Kwandobe Kawe.
Umati wa watu ulijaa maeneo hayo huku wengi wakionesha sura za huzuni na mshutko wakati wakishuhudia tukio hilo la watu wanne kufukiwa na kifusi.
Bado hadi sasa juhudi zinaendelea za kunasuliwa watu waliofukiwa na hata kuangalia kwamba pengine kuna wengine ama la katika eneo hilo la tukio ambalo limevuta mamia ya watu kuliona na kutoa msaada.
Picha kwa hisani ya ITV
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment