Rais wa
Tanzania John Magufuli amepangiwa kufanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi hiyo
tangu kuingia madarakani mwaka jana.
Dkt
Magufuli anatarajiwa kuzuru nchi jirani ya Rwanda Jumatano na Alhamisi,
kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais Paul Kagame.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya Tanzania, Dkt Magufuli
na Bw Kagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha huduma za
pamoja mpakani katika mpaka wa Tanzania na Rwanda.
Baadaye,
wataelekea Kigali ambapo watafanya mazungumzo ya pamoja.
Dkt
Magufuli pia ataweka shada la maua katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya
Rwanda 1994 mjini humo.
“Ikizingatiwa
kwamba hii ndiyo ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu achukue madaraka Oktoba
2015, ziara hii inaashiria umuhimu ambao Tanzania inaweka katika kuimarisha
uhusiano wake na majirani zake.”
Rais
Magufuli amekuwa mapumzikoni nyumbani kwake eneo la Chato, kaskazini magharibi
mwa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment