Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
Imetangaza bei kikomo za mafuta ya Petroli zinazotarajiwa kuanza kutumika 6
Aprili 2016 nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Felix Ngamlamgosi amesema
kuwa Bei za jumla na reja reja kwa Mafuta ya aina zote ikiwamo Petroli na
Mafuta ya Taa zimebadilika ikilinganishwa na Toleo lililopita la Machi 2016.
Amesema kwa Mwezi Aprili bei ya rejareja ya Petroli
imeshuka kwa shilingi 83 kwa lita sawa na sailimia 4.57,ambapo Bei za rejareja za Dizeli na Mafuta ya Taa
zimepanda kwa shilingi 30 kwa lita sawa na asilimia 2.02 na shilingi 36 lita
sawa na asilimia 2.45.
Pia amesema kuwa kwa kulinganisha toleo la mwezi
uliopita bei ya jumla kwa mafuta ya Petroli imeshuka kwa shilingi 82.82 sawa na
asilimia 4.86,ambapo kwa Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa shilingi
29.96 kwa lita sawa na asilimia 2.17 na shilingi 35.93 kwa lita sawa na
asilimia 2.65.
Mabadiliko hayo ni kutokana na Mabadiliko ya bei za
Mafuta katika Soko la Dunia.
Kwa Mujibu ya Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 bei za
bidhaa za Mafuta ya Petroli zitaendelea kupangwa na soko ambapo EWURA
itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za
Mafuta.
Hata hivyo Ngamlamgosi amesema kwamba kwa sasa Kampuni
zote zipo huru kuuza bidhaa ya Mafuta ya Petroli kwa ushindani ilimradi tu
kwamba bei hizo ziwe chini ya bei kikomo yaani(Prince Cap) kama ilivyotolewa na
fomula iliyochapishwa na EWURA na ambayo ilichapishwa kwenye gazeti ya Serikali
No.405/2015 la Mwezi Julai 2015.
Aidha vituo vyote vya Mafuta sasa vinatakiwa
kuchapisha bei za bidhaa za Mafuta katika mabango yanayoonekana na yakionesha
bei ya Mafuta,huku wanunuzi wakishauriwa kuhakikisha kuwa wanunuapo mafuta
wanapata stakabadhi ya malipo ikionesha jina la kituo.
0 comments:
Post a Comment