Watumishi watatu wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba
mkoani Singida wamesimamishwa kazi na kuamriwa kukamatwa,kwa matumizi mabaya ya
madaraka kwa upotevu wa fedha zaidi ya shilingi milioni kumi na nne na laki
tano,ikiwa ni sehemu ya fedha zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya ujenzi wa
hosteli ya wanafunzi wa kike kwenye shule ya sekondari Kinyangiri.
Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari
baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Iramba kukaa kikao cha
dharura Kaimu Mkuu wa Wilaya ya iramba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama
Bw.Christopher Ngubiagai,amesema kamati imeamua kuchukuwa uamuzi huo kufuatia jengo hilo kuchelewa kukamilika
zaidi ya miaka minne na wanafunzi kutembea umbali mrefu na wengi wao wamepata mimba kutokana na kurubuniwa pindi
wanapo rudi nyumbani nyakati za jioni.
katika hatua nyingine bwana ngubiagai amewataja
waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mwandisi Bw.David Malegi,Fundi Sanifu Bw.Hashimu
Ndatwa na amezitaka malaka husika kumkamata aliyekuwa Mratibu wa Mradi
Bw.Jeremia Lubeleje,ambaye kwasasa amehamia Halmashauri ya wilaya ya Masasi
kurudi wilayani Iramba kujibu tuhuma zinazo mkabili.
BONYEZA HAPA->http://www.itv.co.tz/news
0 comments:
Post a Comment