Baadhi ya wakazi Jijini Tanga wameiomba Serikali
kuingilia kati mgogoro unaofukuta baina ya madiwani wa halmashauri ya Jiji la
Tanga kutoka Chama cha Mapinduzi na Chama cha Wananchi CUF- kwa kushindwa kukaa vikao vya kamati za kujadili maendeleo tangu Desemba
mwaka jana.
Hatua hiyo inafuatia kikao cha kwanza tangu uchaguzi
mkuu ufanyikie Oktoba mwaka jana kuahir ishwa baada ya madiwani wa CUF kumkataa Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani
ambaye ni Meya wa Jiji la Tanga , SELEMAN MUSTAPHER wa CCM
wakidai kuwa hakuchaguliwa halali
katika uchaguzi wa nafasi hiyo uliofanyika Desemba 19 mwaka jana .
Wakizungumza kuhusu
sakata hilo, baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga wamekasirishwa na hatua hiyo na
kutaka haki itendeke kwa sababu wanaoathirika na mgogoro huo ni wananchi.
Kamishna wa Chama cha NCCR - Mageuzi Mkoa wa Tanga
, RAMADHAN MANYEKO amesema wakati
umefika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iingilie kati ili kurudisha mchakato wa zoezi
la kuwaletea maendeleo wakazi wa Tanga .
0 comments:
Post a Comment