Mchezaji Yannick Bolasie ametumia shambulizi la
dakika za mwisho kuipatia Crystal Palace goli lililoipa sare ya 1-1 dhidi ya
Arsenal katika mchezo ambao Arsenal iliutawala.
Arsenal ingeweza kushinda kiurahisi na kukwea juu ya
Manchester City na kuitwaa nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi lakini imejikuta
ikibakia katika nafasi ya nne.
Katika mchezo huo Alexis Sanchez alifunga kwa mpira
wa kichwa akiunganisha pande la Danny Welbeck, na kuwafanya the Gunners
kuongoza.
Alexis Sanchez akipiga kichwa cha aina yake kilichojaa wavuni



0 comments:
Post a Comment