Jimbo la magharibi mwa Sudan, Darfur linapiga kura
ya maoni, miaka 13 baada ya kuanza kwa mzozo wa wenyewe kwa wenyewe
uliosababisha watu 300,000 kupoteza maisha.
Kura ya maoni itaamua kama Darfur itakuwa na majimbo
matano au jimbo moja, ambapo raia watakuwa na siku mpaka ya jumatano kuamua.
Kura hii inapigwa wakati kukiwa na hali duni ya
usalama na watu wengi hawajajiandikisha kupiga kura.
Marekani imeeleza hofu yake kuwa kura hiyo haitakuwa
ya haki, lakini Rais Omar al-Bashir amesisitiza kuwa itakuwa huru na haki.
Kura ya maoni ni hatua ya mwisho ya mchakato wa
kuleta amani ambayo makubaliano yake yalitiwa saini mjini Doha kwa kipindi
kirefu waasi wamekuwa wakiomba kuwepo na mamlaka kwenye miji ili kuzuia kile
wanachodai kuingilia kwa mamlaka ya Khartoum kwenye mizozo ya umiliki wa ardhi
0 comments:
Post a Comment