Ikiwa ni siku moja tangu atutoke Nyota wa muziki wa
Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba kipande
hiki cha Video kimeonekana kutumwa kupitia mitandao ya kijamii kikionesha
Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz akiwa na nguli huyo Studio.
Kwa jinsi kipande hiki cha Video kinavyoonekana
kinaashiria kwamba Diamond Pengine alikuwa katika harakati za kufanya wimbo na
Marehemu Papa Wemba Enzi za uhai wake ambapo bado haijafahamika kuwa pengine
papaa alifanikiwa kuingiza Vocal ya wimbo ambao unaonekana kusikika kipande
Diamond akianza nao ama la licha ya sehemu ya Mwisho kusikika sauti kwambali ya
Papa Wemba akisikika kupokea ubeti kutoka kwa msanii wa Tanzania nayeye kuanza
kuimba ambapo haukuisha.
Kwa kipande hiki cha video tutafanya juhudi za
kuzungumza na Diamond Platnumz kujua nini kilikuwa kinaendelea na je
kilifanikiwa kwa kiasi Fulani ama bado yote tutayafahamu.
Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu
Wembadio Pene Kikumba, alianguka jana na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa
maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan
Ivory Coast.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni
14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa
Soukous,
Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani
Afrika na kote duniani.
Msanii huyo nguli mwenye sauti ya kumtoa nyoka
pangoni anasemekana alianza kutetemeka, kisha akaanguka na kuzirai, alipokuwa
akitumbuiza jukwaani Abidjan.
Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake,
alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.
Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele,
Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na
" Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge
Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) ,
"Zania" (Mavuela Somo.
0 comments:
Post a Comment