VIONGOZI wa vyama 13 vya siasa visivyokuwa na
wabunge, wamepongeza hatua ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein ya
kuwateua na kuwajumuisha viongozi wa vyama visivyokuwa na wawakilishi kwenye
Serikali yake, wakisema hatua hiyo imeimarisha demokrasia visiwani humo.
Jumamosi iliyopita Dk. Shein, aliwatangaza viongozi
watatu kutoka vyama visivyokuwa na
wabunge ambao ni Hamad Rashid Mohamed (ADC), Juma Khatib (Tadea) na Said Sudi
(AFP) ambao wamejumuishwa katika Serikali yake.
Vyama vinavyounda umoja huo ni Chama cha Alliance
For Democratic Change (ADC), Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP),
Sauti ya Umma (SAU), Union for Multiparty Democracy (UMD), Chama cha AFP na Chama Cha Kijamii (CCK).
Wenyeviti wa vyama hivyo walitoa pongezi hizo jana
walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari
na baadae kuzindua klabu yao.
Akizungumzia hatua hiyo, Mwenyekiti wa UMD, Kamana
Masoud, alisema umefika wakati wa Rais Dk. John Magufuli naye kuiga mfano wa
Rais Shein kuwateua viongozi kutoka vyama vingine ili washirikiane kuunda
serikali.
0 comments:
Post a Comment