Hakujaripotiwa taarifa zozote kuhusu uharibifu baada
ya kutokea kwa tetemeko hilo la nguvu ya alama 6 katika vipimo vya Richter.
Hata hivyo watu wamelazimika kutoka kwenye nyumba
zao kama tahadhari.
Tetemeko hilo limetokea baharini kutoka pwani ya
eneo la katikati mwa Ecuador lakini hakujatolewa tahadhari yoyote ya kutokea
kwa kimbunga.
Serikali ya Ecuador ilisema Jumatano kwamba inapata
kutafuta dola bilioni moja za Kimarekani kufadhili juhudi za ukarabati kufuatia
uharibifu uliotokana na tetemeko la kwanza lililotokea Jumamosi.
Rais Rafael Correa amesema tetemeko hilo la kwanza
lilisababisha uharibifu wa dola bilioni tatu za Kimarekani.
0 comments:
Post a Comment