Rais Barack Obama amesema anaunga mkono Uingereza
kubaki katika jumuiya ya Umoja wa Ulaya ili kuweza kuchangia katika vita dhidi
ya ugaidi na masuala wahamiaji na utatuzi wa migogoro ya kiuchumi.
Obama ameyasema hayo huku akiwa anaanza ziara yake
nchini Uingereza ambapo ameongeza kuwa uanachama wa Uingereza katika umoja wa
Ulaya una umuhimu mkubwa na endapo nchi hiyo itajiondoa katika umoja huo
itapunguza nguvu katika vita dhidi ya ugaidi duniani, suala la wahamiaji na utatuzi
wa matatizo ya kiuchumi.
Awali Rais Barack Obama ambaye amemaliza ziara yake
mjini Riyadh Saudi Arabia amesema nchi yake na washirika wa nchi za kiarabu
wataendelea kuwa na mshikamano katika juhudi zao za kuliangamiza kundi la dola
la kiislamu pamoja na kuendelea kuongeza mchango wao katika mapambano hayo.
Rais Obama anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa
Uingereza David Cameroon kwa mazungumzo na baadaye chakula cha mchana na malkia
Elizabeth wa Uingereza hii ikiwa ni siku moja baada ya maadhimisho ya miaka 90
ya kuzaliwa kwa MALKIA ELIZABETH.
0 comments:
Post a Comment