Hii nayo imechukua nafasi katika Story za leo licha
yakuwa mara kadhaa umekuwa ukisikia watu wakilalama kwamba wanafika hospitali
kwaajili ya kuchukua miili ya ndugu zao waliofariki dunia na kukuta
imebadilishwa na kupewa mtu mwingie lakini kwa hii ni tofauti kidogo,Ambapo
familia moja iliyokuwa imefiwa na ndugu yao imejikuta imefika Hospitali ya
Muhimbili kuchukua mwili wa ndugu yao Mochwari na kupewa mwili ambao ni wa
familia nyingine ya Kikiristo na Kuzikwa Kiislam Usangi wilaya ya Mwanga Mkoani
Kilimanjaro na wakiislam kuachwa Mochwari ya Muhimbili.
Ningumu kuamini ila yabidi kuamini Mwili wa
Bi.Janeth Teodory ambao ulikuwa umehifadhiwa Hospitali ya Muhimbili mara baada
ya kufariki dunia siku ya Tarehe 8/04/2016
umekutwa umebadilishwa na kupewa familia nyingine iliyokuwa imekuja
kuchukua mwili wa ndugu yao Bi.Amina Sudi aliyefariki Siku ya ijumaa usiku
kuamkia jumamosi ya tarehe 8/4/2016 nakusafirishwa kupelekwa Mkoani Kilimanjaro
kwaajili ya maziko yaliyokuwa yanafanyika Upareni - Usangi Wilyaya ya Mwanga
Mkoa wa Kilimanjaro.
Baada ya miili hiyo kuchanganywa katika sakata hilo
siku ya jumapili tarehe tisa majira ya saa saba mchana taratibu zote ziliweza
kufanyika kwaajili ya familia hiyo ya Sudi kumuhifadhi waliye amini ni mama yao
Bi.Amina Sudi huko upareni huku watu wakilia na huzuni kedekede kwa kujua
mpendwa wao huyo ndiye katolewa jijini Dar es Salaam kwaajili ya maziko.
Kwakuwa Marehemu Amina Sudi alikuwa ni Muislamu basi
taratibu za kuaga hazikuweza kufanyika kama wafanyavyo wakristo kwamba kuna
muda wa kuaga ambao wakati mwingine huchukua hata siku mbili na yatatu kuzika
lakini kwa maiti hiyo ya kiislam ilikuwa ni bandika bandua ambapo hadi
wanakwenda makaburini kuzika bado kulikuwa hakuna utambuzi wa kutosha kuwa
wanaye mzika si ndugu yao wamechanganya mambo.
Baada ya shughuli hiyo ya Maziko kumalizika kila
mmoja wao alirudi kutoka makaburini na kurudi nyumbani palipo na msiba na
kusikiliza kilichokuwa kikiendelea haswa kwa waislam upo ujumbe ambao pia shehe
huutoa kwa watu wote waliohudhuria msiba huo ili wakumbuke kwamba dunia ni
mapito tu na huko ndiko tuendako nashughuli hiyo ikafanyika ikamalizika nawatu
kutawanyika hivyo siku ya jumatatu Tarehe kumi ilitazamiwa kuwa patafanyika
duwa maalumu ya kumuombea Marehemu kabla ya watu wote haswa wanandugu
kutawanyika kuelekea wanapo fanyia kazi na kujipatia riziki za siku.
Ndugu wa
Marehemu Janeth.
Katika Hospital ya Taifa Muhimbili ndugu wa Marehemu
Bi.Janneth Teodory walifika Asubuhi na Mapema kuweza kufanya Taratibu za
kuchukua Mwili wa Mpendwa wao ili waende wakampumzishe huku wakiwa tayari
wamenunua Sanduku la kuhifadhia ndugu yao huyo huku watu huko majumbani wakiwa
katika huzuni ya kusubiri mpendwa wao kwamba sasa analetwa ili taratibu
zikamilike za lini watakwenda kumuhifadhi lakini mambo yakawa tofauti.
Baada ya Kufika Muhimbili sasa hiyo jana tarehe
10/4/2016 na kuulizia Mwili wa mpendwa wao waliibngia ndani na kuoneshwa miili
yliyokuwapo lakini wao hawakujua lolote kwamba kuna kuna mkanganyiko wa mambo
umejitokeza,katika tafuta tafuta waliukosa mwili wa mpendwa wao jambo lililo
wafanya kupigwa na butwaa kwa mpendwa yetu kaenda wapi ama imekuwaje na mawazo
kuwapelekea kwamba huenda kaibiwa.
Sasa baada ya sintofahamu hiyo kujitokeza hiyo
asubuhi basi ikabidi kujua ilikuwaje ambapo kwa wanaohusika nan a Mochwari
wakiwamo wasimamizi ilibidi kuangalia tena ndipo kugundua kwamba walichanganya
mambo na kukuta kwamba Mpendwa wao kasafirishwa kwenda kuzikwa Usangi huko
Upareni tena Kiislam wakati ni Mkristo,na Maiti ya Kiislam kuachwa Dar es
Salaam hali ambayo nawao wasingetazama vyema huenda wangeenda kuizika
Kikiristo.
Baada ya kugundua hivyo Basi familia iliyo pewa
mwili wa Marehemu Janneth kimakosa waliarifiwa hali iliyowafanya kupigwa na
butwaa kwa kilichotokea huku wengine wakistyajabu kwakuwa kwao imekuwa nikama
story tu kuzisikia kwa wengine lakini kwao haikuwahi kutokea.
Taarifa mara baada ya kuwafikia ilibidi tena
taratibu kuanza upya kwa namna ya kuja kuchukua ndugu yao aliyeachwa huku
Mochwari ya Muhimbili lakini kwa Taratibu maalumu huku Mwili wa Marehemu
Janneth ukiwa umezikwa kiislam tayari huko Usangi.
Mpaka usiku wa tarehe 11/04/2016 Taratibu
zilikamilika kwa kupewa vibali maalumu na Polisi huku hospitali ikitoa gari
kwaajili ya kupeleka Mwili uliokosewa huko Usangi – Upareni na Uliozikwa
Kufukuliwa na kurudishwa Dar es Salaam ili ndugu wenye mpendwa wao kuanza
Taratibu upya za Mazishi kisha Maziko.
Tarehe yaleo 12/04/2016,Maziko ya Marehemu Amina
Sudi wa Usangi yanafanyika Tena upya huku Mwili wa Marehemu Janneth Uliozikwa
Kiislamu ukifukuliwa ili kurejeshwa Dar es Salaam na kukabidhiwa ndugu na Jamaa
zao.
Kauli ya Mtoto wa Marehemu Janneth Teodory anasema
kuwa Marehemu alikuwa anasumbuliwa na tumbo pamoja na figo,ambapo alifariki
dunia katika Hospitali ya Muhimbili Tarehe 8/04/2016 na kwamba Tarehe
11/04/2016 walivyofika Muhimbili walikuwa tayari wamekamilisha taratibu zote za
kuuchukua mwili huo kwa ajili ya Mazishi ya Mama yao Mpendwa lakini ndipo wakakutana
na hali hiyo ya utofauti.
Kwa wakati Mwingine ndugu wa Marehemu Janneth
walihoji kuwa yawezekana vipi ndugu kuuchukua Mwili ambao sio wao na wakajiridhisha
ni ndugu yao na wakazika?
Ilikuwaje naye msimamizi wa Mochwari kutoa ndugu
ambaye sio wa wahusika huku wakiwa na alama maalumu mara baada ya kufariki?.
Maswali hayo yalionekana niyautata kwa namna moja
ama nyingine lakini nijambo ambalo limejitokeza na hakuna jinsi kikubwa
nikuchukuliwa Mwili wa Mpendwa wao na kurudishwa.
Wakati wa ufuatiliaji ilibainika kuwa Marehemu hao
wawili Janneth na Amina Sudi mafaili yao yalichanganywa na wahusika wa Mochwari
ambapo hadi dakika za mwisho Process zote zinafanyika kwa Janneth zikijulikana
kuwa ni Amina hali iliyokuwa niyakushangaza na wakati mwingine kuhoji umakini
wa wasimamizi wa Mochwari na hata wahusika wanaiochukua miili yao.
Si leo kusikia miili ikichanganya lahasha ishaa
tokea Mwanza,Tanga na Amana jijini Dar
es Salaam kwa siku za usoni hapa lakini imekuwa Tofauti kwa Mwili wa Kikristo
kuzikwa Kiislam ndipo hapo kumeshangaza ulimwengu na hata ndugu na jamaa wa
Pande Zote.
Kuzungumzia hili na kutaka kujua nikani haya
yanajitokeza katika uchukuaji wa Miili ya Marehemu katika hospitali mbalimbali
nchini Tambarare Halisi Ilibisha Hodi kwa uongozi wa Muhimbili lakini hapakuwa
na Mafanikio ambapo Mkurugenzi wake wa hospitali ya Muhimbili alielezwa kuwa
nje ya Ofisi, licha ya kukiri kutokea tatizo hilo la kutoa maiti kimakosa.
Msimamizi wa Mochwari alijaribu kuztaka kuzungumzia
hali ilivyokuwa lakini aliacha kuzungumza pengine kwa kuhofia kibarua chake na
kudai yeye si mzungumzaji wapo wazungumzaji na hivyo hali ya sinto fahamu
ikaendelea kugubika vichwa vya Ndugu na Jamaa kwa kilichotokea.
Mwili wa Marehemu Janneth unatazamiwa kuletwa leo
baada ya kufukuliwa huko Usangi – Upareni ulipokuwa umezikwa kimakosa tokea
jumapili tarehe 9/04/2016 ambaopo ikiwa hadi hivi leo tarehe 12/04/2016 ni siku
ya Tatu.
Ipo haja pia ya umakini kuwepo wakati wa utambuzi wa
miili ya wapendwa walio fiwa ili kujua bndiye ama siye ili kuepusha minong’ono
na maswali juu ya hili,na Pia wasimamizi katika Mochwari za Hospitali za
Tanzania kuwa na Umakini wakuacha kuchanganya Mafaili ama kuwapiga danadana
watu wanaokuja kuchukua chochote kitu kama baadhi ya wanaokutwa na mikasa hiyo
kusema hali inayokuwaga humo.




0 comments:
Post a Comment