Hali ya taharuki imetokea katika shule ya Mtakatifu
Petro iliyopo Manispaa ya Tabora baada ya Mabweni mawili kuteketea kwa moto
wakati wanafunzi zaidi ya 138 wakiwa darasani.
Inaelezwa kuwa Moto huo ulizuka gafla tu ambapo
sababu za kuzuka kwake hazikufahamika mara moja nahivyo kuunguza mabweni ya
wavulana katika shule hiyo iliyokuwa imejengwa kwa zaidi ya Milioni 70.
Vitu vya wanafunzi vimeshindwa kuokolewa mara baada
ya baada ya gari la zimamoto kuzama eneo la shule hiyo kutokana na ubovu wa
Miundo Mbinu.
Kwa upande wa mkuu wa shule hiyo Bw.Simon Piter Kyalla
akizungumzia sababu za kuzuka kwa moto huo shuleni hapo amesema hajafahamu mara
moja kwani wao wameona tu moto ukiwaka hivyo kukumbusha moja ya tukio lilowahi
kutokea Mwaka jana 2015 ambapo Mabweni mawili moja la wavulana,na la wasichana
kwa nyakati tofauti yaliteketea kwa moto, akidai kuwa ni umeme.
Kufuatia tukio hilo la mabweni kuwaka moto katika
mazingira ya kutatanisha tena mchana kweupe, mkuu wa wilaya ya tabora mjini bw,
suleimani kumchaya ameamua kuifunfa shule hiyo kwa mda usiojulikana akidai
kuwa, mpaka viongozi wa taasisisi hiyo wajihoji, akidai si kila simu ni tatizo
la umeme .


0 comments:
Post a Comment