Hatimaye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT),Prof.
Benno Ndulu (Pichani) inaelezwa kuwa amemuandikia barua Rais wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli kung’atuka nafasi yake hiyo.
Bado hakuna taarifa kamili na ambayo imewekwa wazi
na mamlaka ya juu ila fununu zinadai hivyo,na sababu za yeye kuandika barua
hiyo haijafahamika mara moja lakini tupatapo tutawafahamisha kwa kina.
Katika kauli za Rais wa Tanzania katika kuhakikisha
Tanzania inasonga mbele kwelikweli aliwahi mara kadhaa kusema mtu ambaye
atashindwa kuendana na kasi ya serikali yake nibora akang’atuka mapema kwani
yeye anataka watu wachapakazi.
Rais anataka Tanzania ya viwanda kila Mtanzania
afaidike na raslimali za taifa kwa kuamini kuwa Tanzania inakila kitu hivyo
siyo nchi masikini lakini inahitaji mikakati kabambe,ambapo ameweza kukata
mirija ya ulaji ndani ya serikali na kuhakikisha kodi inakusanywa na wengine
kuchukuliwa hatua za kisheria sambamba na kufuta sherehe mbalimbali ikiwemo za
Uhuru ambazo alisema ni aibu kwa taifa kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru huku taifa
likikabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu ambao kwa kiasi kikubwa unasababishwa
na uchafu,na kuagiza watendaji wote wa halmashauri na manispaa nchini
kuhakikisha wanatayarisha vifaa vya kufanyia usafi ili kila mwananchi aweze
kushiriki.
Katika hatua nyingine pia RAIS Dk.John Magufuli
ameweka tena historia kwa kutangaza kufuta sherehe za maadhimisho ya mwaka huu
ya Muungano ambayo hufanyika kila Aprili 26.
Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa
kutumika kwa ajili ya kugharamia vinywaji, vyakula, gwaride, halaiki, burudani
mbalimbali na hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 2, zitumike
kuanzisha upanuzi wa barabara ya Mwanza – Airport katika eneo linaloanzia Ghana
Quarters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
“Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na
kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za
wananchi,” ilieleza taarifa hiyo ya Ikulu.
Kwa hatua hizo ambazo rais amekuwa akizichukua
zimekuwa zikipongezwa na watu mbali mbali ikiwemo wa chambuzi wa mambo licha ya
baadhi kukosoa lakini Rais husimamia msimamo wakitu anacho kifanya kwa kutaka
Tanzania mpya yenye kasi nay a watu kufanya kazi.
0 comments:
Post a Comment