Wananchi mkoani Shinyanga wameiomba Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina kwa taasisi
na vyombo vya kutoa maamuzi ikiwemo Polisi na Mahakama ili kubaini vitendo vya
rushwa vinavyoendelea kuota mizizi mkoani humo na kusababisha wananchi wa
kipato cha chiini kuishi kwa kunyanyasika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa mkoa wa
Shinyanga wakiwemo wajasiriamali wadogo wanaeleza jinsi baadhi ya watumishi
katika idara mbalimbali serikalini wanavyoendeleza vitendo vya rushwa na kuitaka
TAKUKURU kuacha kufumbia macho jambo hilo kwani linafanyika waziwazi bila
kificho.
Katika Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa mkoani Shinyanga Mkuu wa Taasisi hiyo mkoani humo Bw.Gasto mkono amesema
kuwa taasisi yake mkoani humo imeanza mpango mkakati wa kutoa elimu kwa
wananchi namna ya kuripoti vitendo vya rushwa huku akidai kuwa katika kipindi
cha mwezi wa kwanza hadi wa tatu mwaka huu TAKUKURU imeshawakamata Watumishi wa
Serikali wanne na kuwafikisha mahakamani kwa makosa ya kujihusisha na vitendo
vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kinyume na sheria za nchi.
0 comments:
Post a Comment