Kenya imepata jumla ya dola za kimarekani milioni
625 kwa ajili ya kugharamia mradi wa huduma ya usambazaji wa umeme kufikia
asilimia 70 kwa nchi nzima hadi kufikia mwaka 2017.
Waziri wa nishati na mafuta wa Kenya Bw Charles
Peter amesema serikali imeanza kutekeleza mpango uliopewa jina la "Last
Mile" wenye lengo la kuhakikisha kuwa kila mkenya anapata umeme. Fedha
hizo zimetolewa kwa pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa, Benki ya
Uwekezaji ya Ulay, Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Dunia.
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme la Kenya Dr Ben Chumo
amesema mradi huo unatarajiwa kuhakikisha kuwa kila mwaka wakenya milioni 1
wanapatiwa umeme, na watu wanaoishi umbali wa mita 600 kutoka kwenye vyanzo vya
umeme watapewa huduma hiyo kwa ruzuku.
0 comments:
Post a Comment