Kanali mmoja wa jeshi amepigwa risasi na watu
wasiojulikana katika mji mkuu wa Burundi ,Bujumbura,kulingana na vyombo vya
habari vya kundi la SOS nchini humo.
Kanali Emmanuel Buzubona aliuawa pamoja na mtu mmoja
aliyekuwa akiendesha pikipiki siku ya Jumatano kaskazini mwa makaazi ya mji
huo.
Ni miongoni mwa maafisa wa jeshi wa hivi karibuni
kuuawa tangu rais Pierre Nkurunziza kunusurika jaribio la mapinduzi na
maandamano kufuatia hatua yake ya mwaka jana kujiongezea mda wa kuhudumu kama
rais wa taifa hilo.
0 comments:
Post a Comment