Yanga imeondolewa katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabo 3-2 hiyo ni baada ya jana kufungwa bao la
usiku na kupoteza mchezo kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Borg El Arab jijini
Alexandria nchini Misri.
Mara baada ya mchezo huo ambao wachezaji wa Yanga
walipambana kwa nguvu zote mwanzo mwisho, baadhi yao waliangua kilio mara baada
ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho kutokana na kazi kubwa waliyoifanya kuvurugika
dakika za lala salama.
Al Ahly ndiyo walikuwa kupata bao lakini Yanga
wakasawazisha kupitia kwa Donald Ngoma ambaye alifunga kwa kichwa baada ya
kuunganisha pasi nzuri ya beki wa kulia Juma Abdul.
Beki wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua hakuamini
macho yake na alikuwa mmoja wa wachezaji walioangua kilio mara baada ya mwamuzi
kupuliza kipenga kwa kuwa waliamini mchezo huo ungemalizika kwa sare ya bao 1-1
kisha kuongezwa dakika 30.
Mpaka kufikia dakika ya 90 matokeo yalikuwa 1-1,
mwamuzi wa akiba akonyesha kuwa kuna dakika 5 za nyongeza, wakati huo kwenye
benchi la Al Ahly wote walikuwa katika hali ya taharuki huku wakiwa hawaamini kilichokuwa
kikitokea uwanjani.
Wakati ikionekana sasa mwamuzi anajiandaa kumaliza
mchezo ndopo bao hili likaingia na wachezaji kujikuta wakianza kulia, kiungo
Thaban Kamusoko aliwaongoza katika kuwatuliza.
Yanga sasa itashiriki katika mechi za mtoano za
Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.
0 comments:
Post a Comment