Zaidi ya watoto 4000 huzaliwa na vichwa vikubwa kila
mwaka nchini, lakini wanaorudi hospitali kwa ajili ya tiba kwa kawaida huwa
hawazidi 400, hali inayodhihirisha wanaobaki 3600 hupotea katika jamii hii ni
kutokana na imani za kishirikina ambapo wazazi wengi hudaiwa kuficha watoto wao
na wengine kuwaua kabisa.
Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa kutoka taasisi ya
tiba na upasuaji ya Muhimbili, Othman Kilowoma, alipokuwa akiongea na waandishi
wa habari ofidini kwake jana kuhusiana na kampeni ya Upasuaji wa watoto wenye
vichwa vikubwa na migongo wazi itakayoanza mapema wiki ijayo jijini Mwanza
iliyoratibiwa na kudhaminiwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya GSM Foundation.
"Ni baadhi ya wazazi wenye ujasiri na uelewa tu
ambao huchukua jukumu la kupeleka watoto wao hospitalini au hata kwenye vyombo
vya habari kutaka msaada wa tiba kwa watoto wao kutokana na ughali wa tiba
yenyewe ambapo asilimia kubwa huwa ni upasuaji", alisema Dokta Kilowoma.
Naye muwakilishi wa GSM Foundation, Halfan Kiwamba,
aliwaambia wanahabri kwamba suala la kichwa kikubwa na Mgongo wazi, pengine
nalo lingekuwa na kampeni zake za kitaifa kama ilivyo pepopunda, Malaria,
Magonjwa ya moyo na mengineyo lakini kwa kuwa watoto wanaozaliwa na magonjwa
haya si rahisi kuonekana limekuwa likionekana kuwa ni suala dogo kumbe si dogo
kama tunavyolifikiria.
"Tumeamua kuingia katika mradi huu baada ya
kuona kuwa ni kubwa, na hakuna Taasisi nyingine inaypoliangalia suala hili kwa
upana kama linavyostahili.Gharama za upasuaji kwa mtoto mmoja ni shilingi za
kitanzania laki saba mpaka Milioni moja kulingana na ubora wa vifaa
vitakavyotumika kufanya upasuaji. Ingawa serikali imetamka kuwa na sera ya
kutibu watoto chini ya miaka mitano bure lakini si wote wanaoweza kuhudumiwa
kwa kiwango chenye ubora", alisema Bw Kiwamba.
Changamoto kubwa katika suala hili ni uhaba wa vifaa
na madaktari bingwa, ambao kwa nchi nzima wako TISA tu. NANE wakiwa dar es
Salaam na mmoja anapatikana katika hospitali ya Bugando iliyo kanda ya Ziwa
kule Mwanza.
Baada ya kulifikiria tatizo hili kwa umakini, kwa
kushirikiana na taasisi ya Mifupa na upasuaji, GSM Foundation ilijiuliza
maswali kadhaa likiwemno la jinsi ya madaktari hawa kuwexza kuwafikia wagonjwa
wa mikoani, ambao wengi wao hufichwa ndani kwa kuhofia fikra potofu dhidi yao.
Timu ya Madaktari Bingwa itafika mikoa husika,
kwanza kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya, ya jinsi ya kumhudumia mtoto mwenye
kichwa kikubwa na mgongo wazi lakini pia kufanya upasuaji kwa watoto
watakaojitokeza, kuhudhuria tiba zitakazotolewa na madaktari hao bure.
GSM Foundation kwa kuelewa kwao jinsi Taifa letu
linavyohitaji nguvu kazi ya taifa la kesho imeona si busara kuwaacha watoto
hawa wateketee, na imeamua kuokoa maisha yao.
RATIBA YA KAMBI ZETU KWA AWAMU YA KWANZA NI KAMA
IFUATAVYO:
Mwanza ni April 27 mpaka 30
Shinyanga ni Mei 2 mpaka 4,
Singida Mei 6 Mpaka 8,
Dodoma, Mei 10 mpaka 13
Morogoro mei 15 mpaka 17.
Media Assistant
M Net House, Kawe
P. O. Box 19754
Dar es Salaam, Tanzania
Contacts:
Mr. Henry Mdimu
Managing Director
+255 78 700 0880
+255 71 500 0881
0 comments:
Post a Comment