Kenya sasa inataka faili za kesi zinazowakabili
wakenya watatu wanaotuhumiwa kuingilia ushahidi wa mashahidi wa ICC kushtakiwa
nchini humo.
Mwanasheria mkuu Profesa Githu Muigai amesema kuwa
Kenya ina mahakama zilizo na uwezo za kushtaki kesi ndogo kufuatia kuanguka kwa
kesi kuu iliowahusisha wakenya sita maarufu kama Ocampo 6.
Mwanasheria huyo pia ameshtumu idara ya mashtaka
katika mahakama ya ICC kwa kushindwa kushirikiana na Kenya kuhusu ombi la awali
lililowasilishwa kwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka Moreno Ocampo kuikabidhi
Kenya faili zote za washukiwa.
Amesema kuwa Kenya ina haki ya kushirikiana na
mahakama hiyo au la iwapo ICC itafeli kuikabidhi Kenya faili hizo.
Ameongezea kuwa mpango wa Kenya kujiondoa katika
mahakama hiyo utaangaziwa na Umoja wa Afrika AU na kwamba Kenya kama taifa
haijaanza harakati za kujiondoa.
0 comments:
Post a Comment