Madaktari nchini Kenya wapo katika kufanya juhudi za
namna ya kumsaidia Mwanamke aliyefahamika kwa jina la LYdiah Bonarera (24) aliyejifungua watoto wakike mapacha walioungana kuanzia maeneo ya kifua hadi ya tumbo ili
kuwatenganisha katika Hospitali moja ijulikanayo kama Kisii Level Five Hospital
ilioko huko Nchini Kenya.
Madaktari hao nchini Kenya wanasema kuwa sirahisi
kuwatenganisha mapacha hao kwa mara moja lakini kitu wanachokiangalia kwanza
kwa sasa na kinawaumiza vichwa nikuchunguza namna mapacha hao walivyoungana
kwenye mwili wao na hata baadhi ya sehemu wanazotumia kwaajili ya upumuaji na
mambo mengine wasije kuwatenganisha wakawapotezea maisha.
Kwa upande wa Mama mwenye Mapacha anasema kuwa “jambo
hili limenipa mshtuko mkubwa ila naamini mungu atawavusha watoto wangu katika
jaribu hili gumu japo swala kubwa linalonipa wakati mgumu mimi na mume wangu ni namna ya kupata fedha za upasuaji kwa watoto wetu hawa.
Baba mzazi wa mapacha hao Caleb Osoro ametoa wito
kwa wale wote wenye mapenzi mema kuwasaidia kwa hali na mali kufanikisha
matibabu ya watoto hao .
John Ombogo ni Daktari katika Hospitali hiyo amesema
kuwa hawana imani kama Hospitali yao itaweza kufanya upasuaji mkubwa kwa
mapacha hao hivyo watawahamishia katika hospitali ya Taifa ya Kenya , Kenyatta
National Hospital.
0 comments:
Post a Comment