Wakati Serikali ya Tanzania ikiendelea na Mchakato
wake wa kuwabaini watumishi Hewa kila kona ya nchi ripoti imebaini Idadi kubwa
ya watumishi hewa katika mkoa wa Arusha kutoka 270 na kufikia 350.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud
Felexs Ntebenda alipokuwa akikabidhi taarifa ya uchunguzi wa Tume juu ya
watumishi Hewa Mkoani Arusha.
Idadi kubwa ya watumishi hewa walioongezeka
inaelezwa kuwa wanatokea katika wilaya za Arumeru na Karatu ambapo Katibu
tawala anayeshughulikia na Masuala ya utawala na rasilimali watu Mkoani Arusha
amebainisha hayo.
Mara baada ya kupokea ripoti hiyo ambayo inaonesha
mishahara hewa imefahamika kuwa kuanzia Mwezi July 2014 hadi sasa watu wanalipwa mishara hiyo hewa
amelazimika kutoa siku 14 kwa Wakurugenzi wake kuhakikisha kuwa fedha hizo
zilizotolewa zinarudishwa.
Kutokana na wimbi kubwa la watumishi hewa wakuu
wilaya wametakiwa kuhakikisha ndani ya siku hizo wanampatia taarifa ya hatua za kisheria zilizochukuliwa kwa
watumishi waliohusika .
Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Bw.Adolfu Mapunda
amesema hadi sasa inaonesha kuwa zaidi ya bilion 1.5
zimelipwa kwa watumishi hewa katika Mkoa wa Arusha.
0 comments:
Post a Comment