Na.Devotha Songorwa,Morogoro.
Madereva
wa Daladala Mkoani Morogoro wamegoma kwa zaidi ya saa 9 wakishinikiza
Mamlaka ya udhibiti wa Majini na nchi kavu SUMATRA kuacha vitendo vya
kuwanyanyasa hali iliyo sababisha shughuli za kiuchumi kusimama na
wananchi kupaza sauti zao.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa huo wamesema kuwa
mgomo huo umewaathiri pakubwa na kushindwa kufanya shughuli zao za siku
na kusema kuwa mvutano huo na SUMATRA inabidi uishe mara moja kwani
wanapata shida baada ya kusitisha huduma ya usafiri na kupelekea
usumbufu mkubwa huku wanafunzi nao wakionekana kurandaranda mitaani na
maeneo jirani ya Morogoro baada ya kukosa usafiri uliosababishwa na
mgomo huo.
Mgomo huo sasa umewalazimu wanafunzi na abiria waliokuwa
wanaelekea kufanya mahitaji mbalimbali katika mkoa huo na wengine
kuelekea kazini kulazimika kutembea kwa miguu na wengine kupanda magari
ya mizigo ili kuwahi waendapo na kusababisha usumbufu mkubwa kwa siku
hii ya leo.
Wakizungumza na Tambarare Halisi baadhi ya abiria pamoja
na wanafunzi walioathirika na mgomo huo uliochukua saa tisa wameitupia
lawama serikali kwa kushindwa kushughulikia matatizo ya Madereva hao
mpaka kufikia hatua ya kugoma na kuathiri shughuli mbalimbali za
kimaendeleo mkoani humo.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Madereva
Mkoani morogoro wameelezea sababu za mgomo huo kwakina nakusema kuwa
hadi kufikia hatua hiyo nikutokana na utendaji mbovu wa Afisa mfawidhi
wa SUMATRA Mkoa wa morogoro kukamata hovyo daladala na kisha kuwatoza
faini bila sababu za msingi hali ambayo inawafanya wao wajione hawana
haki yeyote.
Mara baada ya mgomo huo wa Madereva kufukuta kwa Saa 9
ilimlazimu Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bwana.Muhingo Rweyemamu kukutana
na Madereva hao ambapo amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
inawaomba warudishe magari Barabarani kwaajili ya kutoa huduma ya
usafiri kwa wananchi mpaka siku ya juma tatu watakapokutana tena kutatua
kero zinazowakabili.
Home
News
Slider
Mgomo wa Madeva na SUMATRA wafukuta kwa saa 9 na kuathiri shughuli za Kiuchumi Morogoro.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment