Rais Barack Obama wa Marekani amekuwa na mazungumzo
leo(21.04.2016)na viongozi wa mataifa ya ghuba nchini Saudi Arabia ili kuhimiza
kampeni kali zaidi dhidi ya kundi la IS.
Rais Barack Obama anafanya mazungumzo hayo licha ya
mahusiano yaliyoingia doa kati ya nchi hizo na Marekani.
Mikutano hiyo mjini Riyadh leo ililenga katika
kujenga mwendelezo wa mikutano kama hiyo iliyoitishwa mwaka jana Camp David,
eneo la mapumziko ya rais wa marekani katika jimbo la Maryland.
Mikutano hiyo inaakisi juhudi zinazochukuliwa na
Ikulu ya Marekani kuwahakikishia na kufanya uratibu na washirika wake wa
mashariki ya kati ambao ni muhimu lakini wenye shaka shaka ambao wanapinga
mjongeleano wa Obama na Iran pamoja na sera za Marekani kuelekea vita nchini
Syria.
Mkutano na nchi washirika wa Marekani wa baraza la
ushirikiano la mataifa ya ghuba unafuatia mazungumzo ambayo Obama alifanya na
mfalme wa Saudia, Salman jana muda mfupi baada ya kuwasili katika nchi hiyo ya
kifalme.
Mbali na Saudi Arabia , nchi hizo za GCC ni pamoja
na Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, Kuwait, Oman na Bahrain.
Marekani na Iran.
Uungaji mkono wa Marekani katika kuondoa vikwazo
dhidi ya Iran baada ya makubaliano ya mwaka jana ya kinyuklia yameuweka katika
majaribu uhusiano kati ya Marekani na baraza hilo la mataifa ya ghuba
likiongozwa na Saudi Arabia.
Viongozi hao wamejadili pamoja na mambo mengine
mizozo ya kikanda nchini Syria , Iraq na Libya pamoja na njia za kuimarisha
mapambano dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.
Wasi wasi wa mataifa ya ghuba.
Ikulu ya Marekani imesema mkutano huo utajumuisha
vikao vitatu. Cha kwanza ni kuimarisha uthabiti wa kikanda na kingine kitahusu
juhudi za kupambana na ugaidi ikiwa ni pamoja na juhudi za kuliangamiza kundi
la al-Qaeda na wanamgambo wa Dola la Kiislamu.
Saudi Arabia, falme za Kiarabu na mataifa mengine ya
ghuba yanakubaliana na mtazamo kwamba wanamgambo wa IS ni kitisho, na
wamejiunga na kampeni inayoongozwa na Marekani ya kulishambulia kundi hilo.
Lakini wanataka Marekani kufanya zaidi kujaribu kumuondoa madarakani rais wa
Syria Bashar al Assad.
Mataifa ya ghuba pia yana shaka kubwa kuhusiana na
utayari wa Obama kuweza kujadiliana na Iran taifa la Kishia lenye nguvu, na
zinahofia kwamba makubaliano ya mwaka jana ya kinyuklia na jamhuri hiyo ya
Kiislamu yataelekeza katika kuweka uwiano mpya wa misimamo ya kikanda na
kuzigharimu nchi hizo.
Mataifa kadhaa ya ghuba yanayoongozwa na Wasunni
yanaona uungaji mkono wa wanamgambo wa Kishia nchini Lebanon, Yemen na Iraq
kuwa sababu kubwa ya kuwapo kwa mvutano wa kimadhehebu na kutokuwa na uthabiti
katika kanda hiyo.
0 comments:
Post a Comment