MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora jana iliendelea kusikiliza kesi ya
kupinga matokeo ya ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kwa kuwataka mlalamikaji na
mlalamikiwa kuwasilisha vielelezo vya matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliofanyika
Oktoba 25 mwaka jana.
Kesi hiyo No.
2 ya kupinga matokeo ya jimbo hilo ipo chini ya Jaji Fedrind Wambari ambaye
alizitaka pande zote mbili kuwasilisha nakala halisi za matokeo ya uchaguzi,
yaani fomu namba 21B mahakamani kama ushahidi.
Jaji Wambari alisema Jimbo la Kigoma Kusini lilikuwa
na jumla ya vituo 382 vya kupigia kura, hivyo kila upande unatakiwa kuwasilisha
fomu hizo ili mahakama iweze kulinganisha hayo matokeo kwa kila kituo.
Mawakili wa upande wa mlalamikiwa ambaye ni
mbunge,Husna Mwilima (CCM) waliiomba mahakama iwape siku moja ili waweze
kuziandaa fomu hizo na kuziwasilisha mahakamani hapo Aprili 6.
Kutokana na maombi hayo, Jaji Wambari alikubali ombi
hilo na kukubaliana kwa pamoja kesi hiyo kuahirishwa hadi Aprili 6 mwaka huu kwa ajili ya kulinganisha
matokeo yaliyopo katika fomu namba 21B.
Katika kesi hiyo aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo
la Kigoma Kusini,David Kafulila (NCCR-Mageuzi) anawakilishwa na Wakili Profesa
Abdallah Safari pamoja na Tundu Lissu wakisaidiwa na Wakili mwenyeji wa Kigoma,
Daniel Lumenyera.
Upande wa mlalamikiwa, Hasna anawakilishwa na Wakili msomi, Kennedy Fungamtama pamoja na
mawakili wa serikali wanaomwakilisha Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu
wa Serikali ambao ni washtakiwa katika kesi hiyo.
Katika kesi
hiyo, Kafulila anaomba mahakama imtangaze yeye kuwa mshindi kwa mujibu wa
sheria ya uchaguzi kifungu No 112 (c) kwa hoja kwamba yeye ndiye aliyepata kura
nyingi kwa mujibu wa matokeo ya kila kituo kwenye fomu namba 21B na kwamba msimamizi wa uchaguzi alimtangaza,
Husna Mwilima kinyume cha matokeo halisi.
0 comments:
Post a Comment