Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha Shamrashamra za
maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu, ambayo huadhimishwa kila tarehe
26 ya Mwezi Aprili, na badala yake ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya
mapumziko kama kawaida, na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama
katika shughuli zao binafsi.
Kufuatia kuahirishwa
kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa
kutumika kwa ajili ya kugharamia Vinywaji, Vyakula, Gwaride, Halaiki, Burudani
mbalimbali na Hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike
kuanzisha upanuzi wa barabara ya "Mwanza - Airport" katika
eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Barabara hiyo
inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao
unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.
Gerson Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
04 April, 2016
0 comments:
Post a Comment