Kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015
iliyokuwa inamkabili Mbunge wa Jimbio la Vunjo Mh.James Mbatia
ambayo ilifunguliwa na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama cha
Tanzania Labour Party Mh Agustino Mrema imeondolewa mahakamani baada ya
pande zote mbili kukubaliana kumaliza kesi hiyo nje ya mahakama.
Kesi hiyo imeondolewa mahakamani baada ya wakili wa
Mh.Agustino Mrema Mh.January Nkobogho kuwasilisha ombi la mlalamikaji mbele ya
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi Mh Lugalo Mwandambo kumuomba aondoe kesi
hiyo mahakamani kutokana na kuwapo maslahi mapana ya umma.
Wakili Nkobogho amesema kutokana na kesi hiyo kuwa
na maslahi kwa wapiga kura wa Jimbo la Vunjo pamoja na kupunguza gharama kwa
Serikali ya kuendesha kesi hiyo mlalamikaji na mlalamikiwa wameridhiana
kuondoa kesi hiyo mahakamani.
Wakizungumza nje ya mahakama baadhi ya mawakili wa
Mh.James Mbatia, Mh.Mohamed Tibanyendela na Mh.Youngsaviour Msuya
wamempongeza Mh.Agustino Mrema kwa uamuzi wake wa kuridhia kumalizika kwa
kesi hiyo
Naye Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mh.James Mbatia
ameahidi kuendelea na ushirikiano na Mh,Agustino Mrema kwa ajili ya maslahi ya
wananchi wa Vunjo na kuahidi kulipa asilimia 50 ya gharama za mawakili .
0 comments:
Post a Comment