Baada ya kuwa na Msigano kwa muda sasa visiwani
Zanzibar kati ya vyama vilivyo na nguvu kikiwamo cha CUF na CCM mara baada ya
matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 Mwaka jana kufutwa na Mwenyekiti wa Uchaguzi
na hivyo uchaguzi huo kurudiwa Machi 20 2016 na CUF kususia Uchaguzi huo
hatimaye jipu latumbuliwa.
Aliyekuwa mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama
cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ameamua kutumbua jipu ndani ya
Serikali ya Zanzibar baada ya kudai fedha nyingi zilitoroshwa kabla ya uchaguzi
na vigogo wengi wa SMZ wana miliki fedha nje.
Maalim Seif Sharrif Hamad ametoa kauli hiyo visiwani
Zanzibar wakati akiongea na waandishi habari kuelezea mikakati ya Chama cha
Wananchi CUF katika kudai haki ya wananchi wa Zanzibar ambapo amesema kabla ya
uchaguzi baadhi ya viongozi walisafirisha fedha nje ya nchi na wengine kununua
majumba kwa fedha za umma ingawa hakuwataja viongozi hao.
Hatua ambazo CUF imezipanga kuchukua maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF
amesisitiza kuwa njia kubwa itaendelea kuwa ya amani na sio fujo wala vurugu
ikiwa ni pamoja na kufuata utaratibu wa kwenda mahakama za kimataifa ingawa
zina utaratibu wake lakini tayari baadhi ya taasisi za haki za binaadamu
wameanza kulishughulikia suala la uvunjaaji wa haki hizo.
Huu ni mkutano wa pili wa CUF kufanya kuelezea
msimamo wao wa kutoitambua Serikali ya Dk.Ali Mohamed Shein na harakati
wanazozichukua ili kuhakikisha mamauzi ya wananchi ya Ockoba mwaka jana
yanaheshimiwa na kutendeka.
0 comments:
Post a Comment