Madini hayo yalikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) yakitaka kutoroshwa kwenda nje ya nchi bila
kufuata utaratibu wa kisheria na baada ya kukamatwa yametaifishwa na serikali.
Akizungumza jana jijini hapa wakati wa ufunguzi wa
maonesho hayo ya tano ya madini ya vito ya siku tatu, Kaimu Kamishna wa Madini
nchini, Ally Samaje, alisema madini hayo yatapigwa mnada katika maonesho hayo
ikiwa ni sehemu ya kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini.
Samaje alisema hakuna mtoroshaji wa madini anayekuja
kutoka nje bila kuwa na mawasiliano ya Watanzania wenyewe na alisema cha msingi
lazima kila mtu awe mzalendo wa nchi yake na kudhibiti utoroshwaji wa madini.
Alisema hivi sasa serikali haina mchezo na
utoroshwaji wa madini hayo ya tanzanite pamoja na mengine na yeyote
atakayebainika kuhusika na utoroshwaji huo, madini yake yatataifishwa na sheria
kuchukua mkondo wake.
“Suala la utoroshwaji wa madini limekuwa tishio na
sisi tunasema serikali ipo makini na jambo hilo na ikibainika madini
yanatoroshwa yatataifishwa, tunataka madini haya ya tanzanite na mengine
yanufaishe Watanzania wenyewe,” alisema Samaje.
0 comments:
Post a Comment