Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema
kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam
bado linaendelea baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.
Akizungumza leo na waandishi habari ,Makonda amesema
kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya
kutafuta na kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.
Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es
Salaam hakuna kufanya kazi yeyote mpaka wamelize kutafuta watumishi hewa kwa
kutumia malipo ya watumishi kutoka taasisi za fedha
Makonda amesema idadi ya watumishi hewa 71
aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre
Simbachawene ni ndogo katika jiji la Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe
endelevu.
Amesema kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa
wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja wanajisikia vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe
hatua na vyombo vya dola.
Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni
watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana
kuchukua fedha wasioifanyia kazi.
0 comments:
Post a Comment