•Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora,Tom Nyanduga kuwa Mgeni Rasmi
Kamati ya maandalizi ya EJAT 2015 leo limetangaza
majina 84 ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT)
2015. Idadi hiyo ni ongezeko la wateule 31 ukilinganisha na tuzo za 2014 ambapo
wateule walikuwa ni 53 tu.
Pia kamati imeeleza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora, Tom Bahame Nyanduga ndio Mgeni Rasmi kwenye Tuzo
za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT ) 2015 zitakazofanyika kwenye tamasha la usiku la
utoaji wa tuzo hizo Aprili 29, 2016 ,
Dar es Salaam.
Kutangazwa kwa wateule wa EJAT 2015 kunafuatia
kukamilika kwa kazi ya kuzipitia na kuchagua zile zilizo na ubora zaidi
iliyofanywa na jopo la majaji 10 lililokaa mwezi Machi mwaka huu. Majaji hao
ambao ni wataalamu mbalimbali wa masuala ya habari walipitia kazi za kiandishi
zaidi ya 570 zilizowasilishwa kwenye makundi ya kushindaniwa 22 kwenye tuzo za
Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015.
Ripoti ya jopo la majaji hao kuhusu wateule wa EJAT
2015, inaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa kwa wateule kwa upande wa luninga ambapo kuna
wateule 27 kutoka wateule wawili katika
tuzo za 2014. Pia kuna ongezeko kwenye wateule wa redio kutoka 17 hadi 27. Hata
hivyo kwa upande wa magazeti wateule wamepungua kidogo kutoka wateule 34 wa
tuzo za 2014 hadi 32 kwa tuzo za mwaka 2015.
Idadi ya wateule wanawake pia imeongezeka kufikia 28
kutoka wateule 18 kwenye tuzo za EJAT 2014.
Pia ripoti inaonyesha kuongezeka kwa kazi zilizoletwa na redio za
kijamii mwaka huu ambapo baadhi yao zimeweza kutoa wateule kwenye tuzo za EJAT
2015.
Jopo hilo la majaji liliongozwa na mwenyekiti wake,
Bi. Valerie Msoka, wajumbe wengine walikuwa
Dk. Joyce Bazira Ntobi ambaye alikuwa katibu wa jopo, na Ali Uki. Wanajopo wengine walikuwa Jesse Kwayu, Kiondo Mshana, Juma Dihule, Godfrey Nago, Nathan Mpangala na Pili Mtambalike. Waandishi hao 84 wataingia
kwenye kinyang’anyiro cha mashindano ya EJAT 2015.
Majaji hao 10 waliapishwa na Rais wa Baraza la
Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo Machi 11, 2016 kabla ya kuanza kazi hiyo. Hii
itakuwa ni mara ya saba kuwatuza waandishi
waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi chini ya utaratibu wa EJAT.
Sambamba na EJAT, Jopo la wataalam kwa ajili ya Tuzo
ya Maisha ya Mafanikio katika Uandishi wa Habari (LAJA) umeanza kazi ya
kutafuta mteule wa tuzo hiyo kwa mwaka huu ambae atatangazwa wakati wa Tamasha
hilo la usiku. Jopo la LAJA linalongozwa
na Mwenyekiti wake Bi. Lilian Kallaghe lina wajumbe watano ambao ni pamoja na
Hamis Mzee, Fili Karashani, Joseph Kulangwa na Wenceslaus Mushi.
Makundi yaliyoshindaniwa ni yafuatayo:
1. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi na Biashara
2. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na
Utamaduni
3. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Mazingira
4. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya
5. Tuzo ya Uandishi wa Habari za VVU/Ukimwi
6. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watoto
7. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utawala Bora
8. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia
9. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi na
Teknolojia
10 Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi
11. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya ya Mama na
Mtoto
12. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu
13. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi
14. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watu Wenye Ulemavu
15. Mpiga Picha Bora – Magazeti
16. Mpiga Picha Bora – Runinga
17. Mchora Katuni Bora
18. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo
19. Tuzo ya Afya ya Uzazi kwa vijana
20. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na
Uchimbaji Madini
21. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Manunuzi ya Umma
22. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kodi na Ukusanyaji
Mapato
Ifuatayo ni orodha ya wateule wa EJAT 2015 ambao
wanatoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari


0 comments:
Post a Comment