Utumbuaji Majipu ambayo ndio aina aliyoingia nayo
rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuri ya Kutumbua majipu na Kuwashughulikia
watumishi wasio waadilifu katika sehemu zao za kazi pamoja na wale wanaotumia
Vibaya madaraka waliyopewa,kasi hiyo imeonesha kuungwa mkono na Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala baada ya kuwasimamisha kazi wahandisi wanne waliokuwa
wakisimia miradi ya barabara ya manispaa hiyo wakiongozwa na mkuu wa Idara ya uhandisi
Injinia Jaffar Bwigane.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko
amesema wakuu hao wa idara ya uhandisi ambao walikuwa wakisimamia ujenzi wa
barabara hizo wamekuwa wakilalamikiwa kwa muda mrefu kutokana na Usimamizi duni
wa miradi ya barabara ya manispaa hizo ambazo asilimia 98 zimejengwa chini ya
kiwango.
Kusimamishwa kazi kwa watumishi hao kutaenda
sambamba na Uchunguzi wa kuchunguza ni kiasi gani cha hasara kilichosababishwa
lakini pia hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya wahusika akiwepo
Injinia Daniel Kirigiti na Siajali Mahili .
Meya wa Ilalaamesema barabara zote zilizojengwa
chini ya kiwango na kuharibika katika kipindi kifupi wakandarasi waliopewa kazi
hiyo watawajibika kuzitengeneza kwa kutumia Fedha zao.
Kuhusu kuzagaa kwa wafanyabiashara ndogondogo
maarufu kama MACHINGA katika jiji la Dar es Salaam Bw,Kwiyeko amesema wameandaa
mpango mkakati wa kutenga maeneo maalum ili wafanyabiashara hao wafanye
biashara zao bila kusababisha msongamano katikati ya maeneo ya jiji.
0 comments:
Post a Comment