Raia wa Tanzania aliyejiunga na kundi la al Shabaab
la nchini Somalia amenyongwa na kundi hilo kwa tuhuma za ujasusi.
Mtandao wa habari wa Hiiraan Online umeripoti habari
hiyo na kuongeza kuwa, hukumu ya kifo dhidi ya Issa Jemes Mwesiga (27) raia wa
Tanzania aliyejiunga na kundi la sh Shabaab mwaka 2013 ilitekelezwa na kundi
hilo siku ya Jumamosi katika mji wa Jilib, katika mkoa wa Jubba Kati yapata
kilomita 400 kusini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu baada ya mahakama ya
kundi hilo kumpata na hatia ya kuifanyia ujasusi Marekani.
Kwa mujibu wa mtandao huo, jaji wa mahakama hiyo
alisoma hukumu hiyo mbele ya kadamnasi ya watu kabla ya kutekelezwa adhabu hiyo
ya kifo katika uwanja ulio wazi.
Jaji huyo alidai kwenye hukumu yake kwamba,
mtuhumiwa amekiri makosa na hivyo amehukumiwa adhabu ya kifo kwa kupigwa
risasi.
Hadi tunapokea habari hii, serikali ya Tanzania
haikuwa imesema chochote kuhusiana na habari hiyo.
dah
ReplyDelete