Waziri wa fedha wa Namibia Calle Schlettwein amesema
kama ufisadi hautazuiliwa, basi utaharibu maendeleo yaliyopatikana barani
Afrika.
Bw. Schlettwein amesema hayo wakati alipotoa Ripoti
ya nne kuhusu utawala barani Afrika huko Addis Ababa, Ethiopia. Ripoti hiyo
inayopima hatua za kupambana na ufisadi na kuhimiza uelewa wa kimataifa kuhusu
vitendo vya ufisadi ilitolewa kwenye uzinduzi wa wiki ya maendeleo ya Afrika.
Wiki ya maendeleo ya Afrika iliyoandaliwa na Kamati
ya Uchumi ya Afrika na Umoja wa Afrika, ilifanyika kuanzia tarehe 31 Machi hadi
tarehe 5 Aprili. Bw. Schlettwein amesema kiwango cha ufisadi barani Afrika ni
cha juu, hasa katika nchi zinazokumbwa na migogoro na zenye maliasili nyingi.
0 comments:
Post a Comment