Wahanga wa mauaji ya halaiki ya Rwanda chini ya
umoja wao Ibuka, watapata wahudumu wa afya wapatao 3,800 watakaowasaidia
kukabiliana na athari za mshituko waliopata kutokana na mauaji ya halaiki.
Kabla ya hapo Rwanda haikuwa na wahudumu wa kijamii
waliopewa mafunzo ili kuwasaidia wahanga ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994.
Wiki hii Rwanda inaanza maadhimisho ya miezi mitatu
ya mauaji hayo kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweka mashada ya
maua kwenye maeneo ya kumbukumbu, kueleza ilivyokuwa wakati wa mauaji,
mihadhara na kuwasha mishumaa.
Mambo yatakayofuatiliwa zaidi katika maadhimisho ya
mwaka huu ni pamoja na haki, hasa utendaji wa mahakama za Gacaca, mali
zilizoporwa za watoto yatima, na wahusika wa mauaji wanaoendelea kuwa huru
katika sehemu mbalimbali duniani.
0 comments:
Post a Comment