Watu wawili wameaga dunia baada ya kuangukiwa na kifusi kwenye machimbo haramu ya dhahabu hapo juzi huko katika mkoa wa Geita.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kuwa
ajali hiyo ilitokea majira ya alasiri juzi Jumamosi, wakati watu watano
walipokuwa ndani ya machimbo hayo yanayopatikana katika kijiji cha
Busaka katika wilaya ya Chato. Kamanda Mwabulambo ameongeza kuwa mvua
zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya kanda ya ziwa yamedhoofisha kuta
za machimbo hayo ya madini na hivyo kusababisha kuporomoka.Shaaban Ntarambe Mkuu wa wilaya ya Chato ametangaza kufungwa eneo la machimbo hayo. Itafahamika kuwa Geita ni kitovu cha uchimbaji wa madini ya dhahabu nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment