Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amemteua Bw. Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma,
Mkoani Mara.
Bw. Hamphrey Polepole anachukua nafasi iliyoachwa
wazi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Uteuzi wa Bw. Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe
18 Aprili, 2016
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2016


0 comments:
Post a Comment