Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli leo jumanne ( 19/04/2016 ) anatarajiwa kulizundua daraja la
kisasa la Kigamboni.
Daraja hilo la kisasa kabisa lenye urefu wa mita 680
ni kiunganishi muhimu kwa eneo la Kigamboni na Kurasini wilayani Temeke jijini
Dar es Salaam.
Kuzinduliwa kwa daraja hilo kutapunguza msongamano
wa magari na abiria ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakitumia vivuko kuingia na
kutoka Kigamboni.
Wadau mbalimbali wameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii, NSSF kwa kusimamia mradi huo hadi kukamilika kwake.

0 comments:
Post a Comment