Image
Image

Rwanda yashutumiwa na BURUNDI kuhusika katika kasi yakuchochea machafuko nchini Humo.


SERIKALI ya Burundi, imeendelea kuilaumu  Rwanda kwa kile inachodai inachochea machafuko nchini mwao, hali ambayo inahatarisha usalama wa wananchi wao.
Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam juzi, Msemaji wa Serikali ya Burundi, Gervais Abayeho alisema wana ushahidi wa kutosha  Rwanda inatoa mafunzo na kuwapa silaha vijana ili kwani nia ya kufanya mipango ya kupindua utawala  nchi hiyo.
“Kuna vijana wamejisalimisha kwa Serikali ya Burundi na kushuhudia Rwanda ndiyo mfadhili wao mkuu kwa kuwapa mafunzo na silaha ,”alisema Abayeho.
Alisema hata vyombo vya Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU), vilifika Burundi kufanya uchunguzi na kujiridhisha madai hayo yana ukweli.
Alisema askari wa nchi yake, waliwahi kukamata gari linalomilikiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia  Wakimbizi (UNHCR), likiwa limetengenezwa kwa ajili ya kuficha silaha.
Baada ya kulikamata gari hilo likiwa na silaha, dereva aliyekuwa analiendesha alikiri kuingiza silaha kwa mara ya tatu nchini Burundi kabla ya kukamatwa.
Kuhusu hali ya usalama, alisema imetulia na kuwataka wananchi waliokimbia kurudi kujenga nchi yao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment