Serikali ya Uingereza imeanzisha uchunguzi wa
dharura kufuatia ufichuzi kuwa wachezaji nyota wa kandanda nchini humo wamekuwa
wakitumia madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.
Gazeti la Sunday Times limechapisha ripoti ya
uchunguzi iliyothibitisha kuwa sio tu wasakataji dimba bali hata waendesha
baiskeli, wachezaji Kriketi na hata wachezaji wa tenisi wamekuwa wakipokea
matibabu kutoka kwa daktari mmoja ambaye anajulikana kwa kupeana madawa hayo
yaliyopigwa marufuku ya kututumua misuli.
Daktari Mark Bonar ambaye anazahanati yake mjini
London Uingereza amekuwa akiwatoza wachezaji nyota maelfu ya pauni za Uingereza
kwa matibabu hayo fiche ambayo imegunduliwa kuwa ni matibabu ya madawa
yaliyopigwa marufuku na shirikisho la kupambana na madawa haramu WADA.
0 comments:
Post a Comment