Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba amefariki dunia
Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu
Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa
maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan
Ivory Coast.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni
14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa
Soukous,
Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani
Afrika na kote duniani.
Msanii huyo nguli mwenye sauti ya kumtoa nyoka
pangoni anasemekana alianza kutetemeka, kisha akaanguka na kuzirai, alipokuwa
akitumbuiza jukwaani Abidjan.
Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake,
alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.
Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele,
Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na
" Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge
Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) ,
"Zania" (Mavuela Somo.
0 comments:
Post a Comment