IDARA ya Uhamiaji mkoani Tanga imewakamata wahamiaji
haramu 177 walioingia nchini bila vibali.
Kati ya raia hao wa mataifa mbalimbali 22, walikamatwa
kwa kufanya kazi bila kibali kwenye taasisi, mashirika na kampuni za mkoani
hapa.
Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Deodat Bazil,
alisema wapo raia sita wa Tanzania wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na
usafirishaji wa wahamiaji hao.
Aliwataja raia waliokamatwa kwa kosa la kufanya kazi
mkoani humo bila vibali kuwa ni kutoka nchi za Kenya, Ufaransa, Ghana, China,
Uholanzi, India, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Ethiopia.
“Watuhumiwa hao walikamatwa katika kipindi cha
kuanzia Januari hadi Machi, mwaka huu. Kesi zao zipo mahakamani zinaendelea
kutokana na tuhuma zinazowakabili ambazo ni uvunjaji wa sheria za nchi,”
alisema Bazil.
Alisema nchi inayoongoza kwa raia wake kuingia
nchini bila vibali halali ni Ethiopia na katika kipindi cha miezi mitatu
kumekuwa na ongezeko la raia wengine kutoka Somalia, Korea Kusini, Burundi na
China.
Aliomba ushirikiano kwa wananchi ili kuwafichua
wahamiaji haramu waliopo katika maeneo yao ikiwa ni hatua mojawapo ya
kuimarisha hali ya ulinzi na usalama wa raia.
0 comments:
Post a Comment