MKUU wa Mkoa wa
Arusha,Felix Ntibenda amesema idadi ya watumishi hewa mkoani humo imeongezeka
baada ya uchunguzi wa awali huku baadhi ya waliokuwa wakifuja fedha za serikali
kwa kudanganya wakiomba kuzirejesha.
Aidha, amesema mkoa
umepoteza Sh bilioni 1.8 kwa mwaka jana kutokana na kulipa watumishi hewa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Ntibenda alisema hivi sasa
mkoa huo unafuatilia akaunti za watumishi hao hewa ili fedha hizo zirudishwe
serikalini huku watumishi wengine baadhi waliokuwa wakifuja fedha za serikali
kwa kudanganya wakiomba kuzirejesha.
Alisema awali wakati
timu ya uchunguzi aliyoiunda kuchunguza watumishi hewa ilibaini mkoa huo kuwa
na watumishi hewa 270, lakini hadi jana idadi hiyo imeongezeka na kufikia zaidi
ya 300.
Alisema wilaya mbili
za Karatu na Arumeru ndizo ambazo watumishi hewa wameongezeka. “Bado
tunaendelea na uchunguzi na naamini wataongezeka lakini hivi sasa hao watumishi
hewa wanahaha kurudisha fedha za serikali lakini hata kama wakirudisha
watapelekwa mahakamani,” alisema Ntibenda.
Alisema hata kama
fedha hizo watazirudisha, lakini watawafikisha mahakamani na pia wanafuatilia
kujua ni kwa nini wakuu wa idara zao walifahamu udhaifu huo, lakini walikaa
kimya na kuwalipa mishahara huku wakijua kuwa wanaihujumu serikali.
Alisisitiza ni vyema
watu wakaacha tabia ya kujipatia fedha nyingi kwa njia isiyo halali kwani
watumishi hewa wanasababisha fedha za serikali kushindwa kufanya shughuli nyingine
badala yake kupata hasara.
Katikati ya mwezi
uliopita, wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa wapya, Rais John Magufuli aliagiza
waende kufuatilia watumishi hewa katika mikoa yao na hadi sasa wamegundulika
watumishi hewa zaidi ya 4,000.


0 comments:
Post a Comment