Waziri mkuu wa uingereza,David Cameron, ametangaza
takwimu za mapato yake na kodi aliyotozwa katika kipindi cha miaka 6 iliyopita
kufuatia kashfa ya nyaraka za panama.
Ni mara ya kwanza kwa waziri mkuu aliyeko madarakani
kufanya hivyo nchini uingereza..
Waziri mkuu Cameroon
amekuwa akikosolewa tangu nyaraka hizo za siri kufichuka kutoka panama
zinazoeleza kuwa baba yake alianzisha wakfu na kampuni ya hewa nchini panama.
Alikiri kuwa aliuza hisa kadhaa za wakfu huo na
kupata dola za marekani $44,000 kabla kuchaguliwa kuwa waziri mkuu.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa cameron alipokea jumla
ya dola 300,000 za marekani kutoka kwa mama yake mwaka 2011, muda mfupi baada
ya yeye kurithi dola 44,000 kutoka kwa baba yake.
0 comments:
Post a Comment