MOJA ya vyakula ambavyo tumekuwa tukitumia kwa wingi
hasa Watanzania wenye kipato cha kati na chini kabisa ni vyakula vya aina kuu
tatu, Wanga, Protini na Mafuta (Fats).
Na kwa kiwango kidogo sana tunatumia vitamin na
madini katika milo yetu. Moja ya masomo ya chakula tunayofundishwa ni kula mlo
kamili.Watu wengi tumekuwa tukitumia elimu hiyo hadi hapa tulipofika.
Napenda kusema tu kwamba mlo kamili ni kwa ajili ya
mtu mzima ambaye hana ugonjwa wowote na ni kwa yule tu ambaye hataki kula
kiafya.
Napenda kusema haya kwa sababu tumekuwa tukila
vyakula vya namna ile ile lakini tumekuwa tukiugua mno magonjwa mbalimbali
yatokanayo na lishe mbovu. Hadi sasa ugonjwa wa kisukari hapa duniani unaua
zaidi ya ugonjwa wa Ukimwi, swali la kujiuliza je, tumejitenga wapi mbali
katika lishe?
Leo nataka nikueleze kidogo kuhusu sayansi ya
chakula aina ya wanga. Maana kila mtu ninayemwelekeza njia sahihi ya kupunguza
uzito anakwambia nitaishije bila chakula cha wanga? Mwili wako hutumia vyakula
vikuu aina tatu ambavyo ni wanga, protini na mafuta.
Na unatakiwa ujue kuwa gramu moja ya wanga
hutengeneza nishati ya mwili kalori nne, ambapo protini nayo hutengeneza kalori
nne na Fats hutengeneza kalori tisa. Unaona ni zaidi ya mara mbili ya nishati
zinazotengenezwa na chakula cha wanga.
Hii ina maana kuwa ninaposema kuwa tunaweza
kupunguza wanga na ukaishi ukiwa na nguvu nyingi zaidi hata ya ulivyo kuwa
katika lishe ya wanga nyingi.
KWANINI NAKUSHAURI UPUNGUZE WANGA KIAFYA?
Unapokuwa umepunguza wanga au kuacha kabisa ulaji wa
vyakula vyenye wanga nyingi, mfano mikate, ugali, wali na tambi. Hakikisha
kitendo hicho kiendane na kuongeza kiwango cha mafuta na vyakula vya protini
mwilini mwako katika lishe yako. Hii itaufanya mwili wako kuanza kutumia mafuta
kama nishati ya mwili ya kwanza kujitengenezea nguvu.
Viungo vya binadamu kama ini na figo vinapokuwa
vinatumia mafuta kuzalisha nishati ya mwili hutengeneza viini vya nishati
viitwavyo Ketone Bodies, ambavyo hivi ndivyo hutumiwa na seli za mwili
kujitengenezea nishati kwa wingi.
Hivyo basi, unapokuwa unajizuia kutumia vyakula vya
wanga mwili wako utatumia karibia siku tano hadi wiki kuanza kutumia mafuta
kama nishati ya mwili na hicho kitendo tunaita Keto Adaption.
Ningependa kusema kwamba Keto Adaption ni ile hali
ya mwili wako kujenga mazoea ya kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwili
na hapo ndipo utaanza kuona mabadiliko katika mwili wako makubwa.
Utakuwa unajisikia mwenye nguvu na unatashangaaa
dalili mbalimbali zilizokuwa zinakusumbua zinapotea hii ni kwa sababu ya uwezo
mkubwa wa ketone bodies katika mwili wako dhidi ya glucose.
Sote tunajua kwamba ulaji wa vyakula vya wanga kwa
wingi na vyakula vyenye sukari nyingi vinaongeza kiwango cha sukari kwenye damu
zaidi ya kiwango ambacho mwili wako unaweza kuhimili.
Mfano; kiwango cha kawaida cha sukari
kinachohitajika mwilini mwako ni kijiko kimoja cha chai, hiki ni kiwango
ambacho hakiwezi kukuletea matatizo. Basi kama binadamu anaishi kwa sukari
inayokadiriwa kuwapo kwenye damu kama kijiko kimoja tu cha chai.
Unywaji wa soda moja unaweza kuongeza zaidi ya
vijiko 10, hivyo basi mwili wako unakuwa unashindwa kuhimili sukari iliyozidi.
Kwa wale wanaopenda kula baga, inakadiliwa kuwa baga
moja ya kati inaweza kutoa sukari zaidi ya vijiko 16 kwenye damu.
Swali la kujiuliza mwili unapeleka wapi sukari
iliyozidi wakati miili yetu inahitaji sukari kiwango kidogo kama kijiko kimoja
tu kuishi?
Mwili hutengeneza maji kutoka kwenye seli za kongosho ziitwazo beta seli, maji haya ni
homon iitwayo Insulin, kazi kubwa ya insulin ni kutunza glucose hii katika damu
kwa matumizi ya baadae, na inatunza katika kiasi maalumu katika mfumo wa
Glycogen na kiasi kikubwa katika mafuta.
Hivyo basi, mafuta haya huhifadhiwa katika sehemu
mbalimbali kama tumboni, shingoni, mikononi, kifuani na kiunoni. Mafuta haya
huhifadhiwa katika mfumo wa Tryglycerides ambayo haya ni miongoni ya mafuta
mabaya mwilini mwako.
Sasa mtu anayekwambia wanga nyingi katika chakula
chako ni salama anakudanganya kwa kiasi kikubwa kwani tunaona jinsi gani ulaji
wa kiwango kingi cha vyakula vya wanga na sukari vinavyosababisha sukari
kupanda kupita kiasi na insulin kuanza kuhifadhi katika mafuta.
Kila siku nasema, tumekaririshwa adui mkuu ni fats
na kujisahau ulaji mbovu wa vyakula vya wanga huku tukiishia kulea vitambi na
magonjwa sugu, hii yote ni kutokuwa na ufuatiliaji wa lishe nzuri na salama
kwako.
MADHARA MENGINE YA SUKARI
Napenda kuwarudisha nyuma kidogo katika somo la
bailojia. Tulijifunza kuwa miili yetu imejengwa kwa kiini kidogo sana kiitwacho
seli ambapo shughuli zote za mwili zinafanyika humo.
Nilijifunza kuwa ndani ya seli kuna viungo vidogo
vidogo navifananisha na (Apartments
kwenye nyumba kubwa) moja wapo ni Mitochondria, hiki ni kiungo kidogo
katika seli ambacho kinahusika na kuzalisha nishati ya mwili tu. Pia
nikikumbuka watu wote tulijifunza kwamba mwili wetu hujitenegenezea nishati ya
mwili au nguvu kupitia kuifanyia kazi sukari iliyo ndani ya damu baada ya
kuingia ndani ya seli.
Hivyo basi insulin ni kama ufunguo ambao unafungua
milango ili sukari iweze kuingia ndani ya seli hadi kwenye mitochondria. Mwili
wako unapokuwa unatumia hewa ya oxygen kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa athari
iitwayo Oxdative stress.
Hii ndiyo inayofanya chuma kipate kutu, hii ndiyo
inayofanya mafuta ukiyaweka kwenye jua kwa muda mrefu yanaharibika. Basi mwili
wako unakuwa unatengeneza vihatarishi viitwavyo Reactive Oxygen Species kwa
kifupi huitwa Free Radicals.
Hizi ni sumu ambazo hupatikana wakati mwili
unajitenegenezea nishati yake kwa kutumia oxygen na hizi zinapokuwa kiwango
kikubwa huweza kuharibu kabisa seli na kuziua na pia zinaweza kupelekea kupata
magonjwa sugu kama saratani.
Hivyo, tafiti zinaonesha kwamba vyakula vya wanga na
sukari vina matokeo makubwa ya kutenegeneza Free Radicals nyingi kupita kiasi.
Miili yetu ina kiwango fulani cha viondoa sumu
ambavyo vinaipunguza sumu ya free
radicals kuepusha kusababisha magonjwa kwa kuziua seli.
Lakini panapokuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji
wa free radicals mwili unashindwa kuhimili na hatimaye free radicals zinaanza
kuleta madhara mwilini mwako. Kadri mitochondria zinavyodhoofika ndivyo
magonjwa nyemelezi ya lishe yanavyotukabili kila kukicha.
0 comments:
Post a Comment