Image
Image

BUNGE lafanya mabadiliko ya Kamati zake za Kudumu kwa mara ya nne.

BUNGE limefanya mabadiliko ya Kamati zake za Kudumu kwa mara ya nne tangu kuundwa kwake ambayo yamemrudisha Andrew Chenge katika Kamati ya Bajeti kama Mjumbe Mwalikwa.
Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga alitangaza mabadiliko hayo kwa wabunge jana jioni, lakini hakutaja sababu za mabadiliko hayo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bunge, wabunge sita akiwamo Chenge ambaye ni Mbunge wa Bariadi (CCM), wamepelekwa kuwa wajumbe waalikwa katika Kamati ya Kudumu ya Bajeti.
Chenge aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali anatoka katika Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo na katika Bunge la 10 alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti. Wengine waliopelekwa Kamati ya Bajeti pamoja na Chenge na kamati zao katika mabano ni Joseph Selasini (Serikali za Mitaa) na Dk Dalaly Kafumu (Viwanda, Biashara na Mazingira).
Hao ni Japhet Hasunga (Hesabu za Serikali - PAC), Albert Ntabaliba (Uwekezaji - PIC) na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu (Huduma na Maendeleo ya Jamii). Wabunge waliohamishwa Kamati na kamati za awali na wanazokwenda katika mabano ni Ezekiel Maige (Nishati na Madini – PAC), Allan Kiula (Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama – PAC), Omary Mgumba (Sheria Ndogo – PAC), Rhoda Kunchela (Masuala ya Ukimwi – PAC), Joseph Kakunda (PIC- PAC).
Wengine ni Ahmed Ally Salum (PAC – Huduma na Maendeleo ya Jamii), Neema Mgaya (Huduma na Maendeleo ya Jamii – Ardhi, Maliasili na Utalii) na Salma Mwassa (Bajeti – Ardhi, Maliasili na Utalii).
Aidha, taarifa hiyo ilieleza kuwa wabunge wawili akiwamo Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga na Dk Hadji Mponda wameondolewa katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment