SERIKALI imesisitiza kuwa haitaongeza muda wa kuzifungia simu feki ifikapo Juni 16 kwani inataka Watanzania wajifunze kufuata taratibu. Aidha, imesema itatoa muongozo wa namna ya kuzitupa simu hizo kwa kuwa ni taka maalumu ambazo hazitakiwi kutupwa hovyo.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na huduma ya 4G LTE.
Profesa Mbarawa alisema kuwa ufungiaji huo unalenga kuhakikisha kuwa simu na vifaa vyote vya mawasiliano vinavyotumika nchini, vinakuwa halisi vyenye ubora na vinavyokidhi sifa za huduma.
Aliwataka wananchi kuzingatia kikamilifu maelekezo yanayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu namna ya kuzitambua simu feki. Akizungumzia uzinduzi wa nembo hiyo, Profesa Mbarawa alisema kuwa serikali itaiwezesha TTCL kwa kuiongezea masafa ya megahezi 800 waweze kuingia katika soko la ushindani la mawasiliano nchini.
Alisema awali waliipa TTCL megahezi 1800 ambazo zimesaidia kuingia katika mtandao wa kasi wa 4G LTE kwamba kampuni hiyo pekee haiwezi kununua masafa hayo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema kuwa wameboresha miundombinu ya simu za mezani na mkononi kwa kuleta teknolojia ya 2G GSM, 3G UMTS na LTE sokoni kwenda sambamba na ushindani
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment